超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Rwanda yashuhudia maendeleo katika kukabiliana na ugonjwa wa Marburg

(CRI Online) Oktoba 21, 2024

Waziri wa Afya wa Rwanda Bw. Sabin Nsanzimana amesema kwa muda wa siku tano zilizopita hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya Marburg (MVD) nchini humo, hali inayoashiria kuwa hatua kubwa zimepigwa katika mapambano dhidi ya virusi hivyo nchini Rwanda.

Bw. Nsanzimana ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano na wanahabari mjini Kigali, wakati nchi hiyo ikiendelea na juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

Amesema kati ya watu 62 walioambukizwa ugonjwa huo, 15 wamefariki dunia na wengi wamepona, kwa sasa ni wagonjwa watatu tu ambao bado wanaendelea na matibabu.

Dk. Nsazimana amesema Rwanda itaendelea kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuimarisha ufuatiliaji na mwitikio, ili kuhakikisha inajiandaa vizuri dhidi ya uwezekano wa kutokea kwa maambukizi yoyote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha