超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Zimbabwe kuimarisha ushirikiano wa FOCAC kwa ajili ya mambo ya kisasa

(CRI Online) Septemba 26, 2024

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa nchi hiyo itaimarisha ushirikiano ulioanzishwa chini ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ili kuharakisha mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa, mapinduzi ya viwanda na kutekeleza mageuzi ya kiuchumi yanayozingatia watu.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 378 wa Chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF mjini Harare, Rais Mnangagwa amesema kuwa, ziara yake ya kiserikali nchini China na kushiriki katika mkutano wa FOCAC imetoa fursa ya kuimarisha uhusiano kati yake na China katika nyanja mbalimbali.

Rais Mnangagwa pia amesema licha ya kuangazia uchumi na biashara, ni muhimu kutafuta ushirikiano na China katika sekta nyingine zikiwemo michezo, utamaduni, utalii na vyombo vya habari.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha