超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Kenya yaahidi kuongeza hatua kuboresha uhifadhi wa faru

(CRI Online) Septemba 23, 2024

Kenya imeungana na jamii ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Faru Duniani, huku ikiahidi kuimarisha hatua za kuokoa idadi ya Faru weusi nchini humo.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku hiyo yaliyofanyika kitaifa katika Kaunti ya Samburu, kaskazini mwa Kenya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Wanyamapori nchini Kenya, Rebecca Miano amesema serikali imetekeleza matumizi ya teknolojia mbalimbali ikiwemo droni na ushahidi wa kimahakama ili kuongeza ulinzi wa Faru.

Pia amesema, serikali imetenga rasilimali muhimu ili kusaidia ajira kwa maofisa zaidi wa sheria, hatua ambayo itatoa mchango mkubwa katika juhudi za kuokoa idadi ya Faru iliyopo sasa na wanyamapori wengine kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Amesema Kenya ni makazi muhimu ya Faru, ikiwa na asilimia 80 ya Faru weusi wa mashariki wanaopatikana katika maeneo manane nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha