超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Kampuni za dawa na nishati za China zaunga mkono juhudi za maendeleo ya viwanda Zanzibar

(CRI Online) Agosti 09, 2024

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nchini Tanzania imesaini makubaliano siku ya Jumatano na kampuni mbili zinazowekezwa na China ili kuimarisha maendeleo ya sekta ya afya na nishati katika visiwa hivyo.

Kampuni ya dawa ya China, Africa Bio Chem, imesaini makubaliano ya kujenga kituo cha kuzalisha dawa na chanjo. Kampuni nyingine ya China inayojishughulisha na uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua ya ABC Power Tech Ltd, pia inashirikiana na serikali ya Zanzibar kuzalisha umeme wa megawati 200 katika eneo la viwanda.

Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi alishuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo ya uwekezaji, akisema kampuni hizo mbili za China zitakuwepo katika eneo jipya la viwanda la Zuze lililopo Dunga.

Rais Mwinyi ameishukuru China kwa kupeleka dawa nyingi, kutoa mafunzo kwa watu wake na kuwajengea uwezo wananchi, akisema wanatarajia kuendeleza ushirikiano huo.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, mshauri mkuu wa wanasayansi wa kampuni ya Africa Bio, Chem, Yang Chen, amesema kampuni yake imeamua kuungana na Zanzibar kujenga kituo hicho ili kuchangia nguvu zake katika kuboresha kiwango cha afya katika visiwa hivyo na kanda nzima ya Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha