超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Misri wafanya mazungumzo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati

(CRI Online) Agosti 07, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Misri Badr Abdelatty siku ya Jumanne.

Katika mazungumzo hayo, Wang amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa marais wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Misri umepata maendeleo makubwa, na upo katika kipindi bora zaidi katika historia.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Wang amesema mauaji dhidi ya kiongozi mkuu wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran yamefanya hali ya eneo hilo kuwa hatari zaidi, na China inapinga na kulaani vikali vitendo hivyo vya mauaji vinavyokiuka misingi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, mamlaka na hadhi ya Iran, na pia kudhoofisha sana juhudi za kuhimiza amani, na kufanya usimamishaji mapigano huko Gaza kuzidi kushindwa kufikiwa.

Amefahamisha kuwa China itaimarisha mshikamano na nchi za Kiarabu, na kufanya kazi na pande zote ili kuepusha kuongezeka kwa mgogoro na kuzorota zaidi kwa hali iliyopo.

Kwa upande wake, waziri Abdelatty amesema kuwa Misri inathamini mchango muhimu wa China katika kuhimiza amani Mashariki ya Kati, na kushukuru juhudi za China katika kuendeleza maridhiano ya ndani huko Palestina.

Ameongeza kuwa Misri itadumisha ushirikiano wa karibu na China ili kuzuia kuongezeka zaidi kwa hali hiyo mbaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha