超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Wacheza tenisi wa China waweka?historia, Biles aipa Marekani medali ya pili ya dhahabu kwenye mchezo wa jimnastiki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2024

Zheng Qinwen wa China akishindana kwenye nusu fainali ya mchezo wa tenisi kwa mchezaji mmoja mmoja kwa wanawake dhidi ya Iga Swiatek wa Poland kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris Agosti 1, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

PARIS – Mcheza tenisi kipenzi wa China Zheng Qinwen amemhudhunisha mchezaji wa nafasi ya kwanza duniani Iga Swiatek wa Poland na kufika fainali ya mchezo huo kwa mchezaji mmoja mmoja kwa wanawake, huku wenzake Wang Xinyu na Zhang Zhizhen pia wakiweka historia kwa kuingia fainali ya mchezo huo kwa wachezaji wawili katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris iliyofanyika Alhamisi.

Ushindi huo unamaanisha matokeo bora zaidi ya China katika mashindano hayo mawili ya Michezo ya Olimpiki, baada ya mshindi mara mbili wa Grand Slam, Li Na kumaliza wa nne katika mashindano ya tenisi ya mchezaji mmoja mmoja kwa wanawake iliyofanyika kwenye Olimpiki ya Beijing Mwaka 2008.

Baada ya ushindi mgumu wa seti tatu dhidi ya mkongwe wa Ujerumani Angelique Kerber katika robo fainali Jumatano, mshiriki huyo wa fainali ya Australian Open Zheng amepambana zaidi na kumshinda Swiatek kwa 6-2, 7-5 dhidi ya Roland Garros, na kuhitimisha kushindwa kwake mara sita mfululizo kwa mshindi huyo wa mara nne wa French Open.

Wang Xinyu (Kushoto)/Zhang Zhizhen wa China wakiwa katika mapumziko mafupi kwenye nusu fainali ya mchezo wa tenisi kwa wachezaji wawili dhidi ya wawili kwa wanawake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, Agosti 1, 2024. (Xinhua/Wan Xiang)

Wachina wawili Wang na Zhang wamewashinda Demi Schuurs na Wesley Koolhof wa Uholanzi kwa 2-6, 6-4, 10-4 katika nusu fainali ya wachezaji wawili kwa wanawake.

Wang/Zhang watachuana na wachezaji wawili wa Czech, Katerina Siniakova na Tomas Machac katika fainali siku ya Ijumaa.

Mapema siku ya Alhamisi, mshikaji rekodi ya Dunia Yang Jiayu wa China alijinyakulia medali ya dhahabu ya kwanza ya riadha ya China katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, akishinda mbio za kutembea kwa kasi za kilomita 20 kwa wanawake kwa muda wa saa moja, dakika 25 na sekunde 54. Brian Daniel Pintado wa Ecuador amemaliza wa kwanza katika mbio hizo za kutembea kwa kasi kwa wanaume kwa muda wa saa moja, dakika 18 na sekunde 55.

Katika Kituo cha Kulenga Shababa kwa Kufyatua Risasi cha Chateauroux, mchezaji wa China Liu Yukun ameshinda medali ya dhahabu katika mchezo wake wa kwanza wa Olimpiki baada ya kushinda nafasi 3 za kufytaua risasi kutoka bunduki ya rifle kwa wanaume kutoka umbali wa Mita 50 kwa kupata? pointi 463.6, akifuatiwa na Serhiy Kulish wa Ukraine na Swapnil Kusale wa India katika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

Simone Biles wa Marekani akishindana kwenye fainali kuweka mizania ya mwili ya mchezo ya jimnastiki ya pande zote kwa wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, Agosti 1, 2024. (Xinhua/Cheng Min)

Simone Biles wa Marekani akishindana kwenye fainali kuweka mizania ya mwili ya mchezo ya jimnastiki ya pande zote kwa wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, Agosti 1, 2024. (Xinhua/Cheng Min)

Kwingineko, bingwa mtetezi wa Dunia Biles mwenye umri wa miaka 27, ambaye alishinda medali ya dhahabu kwa pande zote huko katika Olimpiki ya Rio 2016 lakini akajiondoa kwenye mashindano ya Tokyo miaka mitatu iliyopita, ametwaa tena taji hilo mjini Paris 2024 kwa pointi 59.131, 1.199 mbele ya mshindi wa medali ya fedha Rebeca Andrade wa Brazil, huku medali ya shaba ikienda kwa mchezaji mwingine wa Marekani, Sunisa Lee.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha