超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Baraza?la Hong Ting lafanyika nchini Kenya kuhusu kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika ili kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 01, 2024

Watu wakishiriki kwenye Baraza la Hong Ting jijini Nairobi, Kenya, tarehe 31 Julai 2024. (Xinhua/Han Xu)

Watu wakishiriki kwenye Baraza la Hong Ting jijini Nairobi, Kenya, tarehe 31 Julai 2024. (Xinhua/Han Xu)

NAIROBI – Baraza la Hong Ting, lenye kaulimbiu ya "China na Afrika Kushikamana Pamoja Kujenga Mambo ya Kisasa," limefanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi siku ya Jumatano, likivutia washiriki kadhaa, wakiwemo watunga sera, wanadiplomasia, maofisa wakuu wa sekta ya viwanda, waandishi wa habari na wasomi.

Baraza hilo lililoandaliwa na Shirika la Habari la China, Xinhua Kanda ya Afrika, limejadili njia zenye uvumbuzi za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali na kufanikisha ujenzi wa mambo mapya.

Kumekuwa na makubaliano kati ya washiriki katika baraza la Hong Ting kwamba Afrika na China zina matarajio ya pamoja ya kupata ustawi na kufikia ujenzi wa mambo ya kisasa kwa kutumia kikamilifu fursa za ushirikiano na kufunzana.

Cavince Adhere, msomi wa uhusiano wa kimataifa wa Nairobi, amebainisha kuwa ushirikiano wenye manufaa kati ya China na Afrika utajenga msingi wa kukuza uchumi wa kisasa, kutoa fursa za ajira na kupanua ustawi kwa usawa.

Huku akitambua mchango mkubwa wa China katika uchumi wa Afrika, Adhere ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano katika ujumuishaji wa kidijitali, mageuzi ya uchumi wa kijani, uhamishaji wa teknolojia, afya, kilimo na usalama ili kutimiza kunufaishana.

Steve Zhao, ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya MOJA Expressway, ambayo ni kampuni tanzu ya China Road and Bridge Corporation (CRBC), amebainisha kuwa kwa kutumia kikamilifu fursa za teknolojia, mitaji na utaalamu wa China, nchi za Afrika zitanufaika na ujenzi wa mambo ya kisasa unaotokana na kuboresha mitandao ya mawasiliano.

Barabara Kuu ya Nairobi yenye urefu wa kilomita 27.1, iliyojengwa na CRBC kupitia ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi na ambayo sasa inaendeshwa na MOJA, imekuza ujenzi wa mambo ya kisasa wa Kenya kupitia usafirishaji wa watu na mizigo, Zhao amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha