超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

China inapenda kuzidisha ushirikiano wa ngazi?ya juu na IOC: Makamu Rais wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2024

Makamu Rais wa China Han Zheng, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, akikutana na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Thomas Bach mjini Paris, Ufaransa, Julai 27, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

PARIS - China inapenda kuzidisha na kupanua ushirikiano wa ngazi ya juu na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), wakati ambapo nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa Michezo ya Majira ya Baridi ya Asia mwaka ujao, Makamu Rais wa China Han Zheng amesema mjini Paris siku ya Jumamosi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa IOC, Thomas Bach.

Han amewasilisha salamu za Rais Xi kwa Bach na kuipongeza IOC kwa mafanikio ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris Mwaka 2024.

Michezo ya Olimpiki inalenga kulinda amani ya dunia na kuhimiza umoja wa binadamu, amesema Han, huku akibainisha kuwa Michezo ya Olimpiki ya Paris ina umuhimu mkubwa kutokana na haja ya kuendeleza moyo wa Olimpiki chini ya hali ya sasa ya kimataifa.

Amesisitiza kuwa China daima imekuwa ikiunga mkono kwa dhati maendeleo ya Kazi za Kimataifa za Olimpiki na imedumisha uhusiano mzuri wa muda mrefu na IOC.

Kwa upande wake Rais Bach amemwomba Han kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi, na amekaribisha kwa furaha ushiriki wa Han kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris kama mwakilishi maalum wa Rais Xi.

Dhamira Kuu ya Olimpiki ya kimataifa kimsingi imejikita katika ushirikiano wa pande nyingi, amesema Bach.

“China daima imekuwa ikiunga mkono dhamira kuu ya Michezo ya Olimpiki ya kimataifa,” amesema Bach, akibainisha kuwa mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing Mwaka 2022 chini ya janga la UVIKO-19 kuliweka mfano wa kuigwa kwa nchi kote duniani wa jinsi ya kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki.

Bach amesema IOC inapenda kuendelea kushirikiana kwa karibu na China ili kuandaa kwa mafanikio michezo mbalimbali ya kimataifa na kueneza maadili ya Olimpiki.

Makamu Rais wa China Han Zheng, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, akikutana na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Thomas Bach mjini Paris, Ufaransa, Julai 27, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Makamu Rais wa China Han Zheng, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, akikutana na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Thomas Bach mjini Paris, Ufaransa, Julai 27, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha