超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China utaanzia Machi 4 hadi 10

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 04, 2024

Liu Jieyi, spokesperson for the second session of the 14th Chinese People's Political Consultative Conference (CPPCC) National Committee, attends a press conference at the Great Hall of the People in Beijing, capital of China, March 3, 2024. (Xinhua/Li He)

Liu Jieyi, msemaji wa mkutano wa pili wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) akishiriki kwenye mkutano na waandishi habari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 3, 2024. (Xinhua/Li He)

BEIJING – Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambalo ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, unaanzia leo Jumatatu Machi 4 saa 9 alasiri (kwa saa za Beijing) hadi asubuhi ya Machi 10 mjini Beijing, msemaji wa mkutano huo Liu Jieyi alisema siku ya Jumapili kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Liu amesema kuwa maandalizi yote ya mkutano huo wa pili wa baraza hilo yamekamilika, na shughuli mbalimbali zimepangwa. Mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China watahudhuria kwenye mkutano huo wa kufunguliwa na kufungwa.

Mwanzo Mzuri

Msemaji huyu amesema, kukumbuka kazi ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ya Mwaka 2023, ambayo inaonesha mwanzo wa kazi ya awamu ya Kamati ya Kitaifa ya 14 ya baraza hilo, amesisitiza kwamba umekuwa mwanzo mzuri. Amesisitiza tena kuwa kazi ya baraza hilo ilikamilika chini ya uongozi mzima wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Liu amesema, katika mwaka uliopita, washauri wa kisiasa walijikita katika kutoa mapendekezo kwa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, ambapo shughuli za mashauriano jumla ya 94 zilifanyika mwaka mzima, zikihusu mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunda muundo mpya wa maendeleo, huku shughuli 138 za utafiti na ukaguzi zikifanywa na washauri hao wa kisiasa.

Maendeleo yenye ubora wa hali ya juu

Msemaji Liu amesema, masuala ya kiuchumi yamekuwa kipaumbele cha juu kwa washauri wa kisiasa wa China katika kutekeleza majukumu yao ya mashauriano ya kisiasa. Baraza la masharuaino ya kisiasa limeshiriki katika mashauriano na kutoa mapendekezo kuhusu masuala mbalimbali ya uchumi na mengine muhimu ya kiuchumi, hasa linafuatilia zaidi maendeleo yenye ubora wa hali ya juu.

Baraza la mashauriano ya kisiasa limetambua kuwa sekta ya kibinafsi ni msukumo wenye nguvu kubwa kwa maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China na ni msingi muhimu wa maendeleo yenye ubora wa hali ya juu, kamati kuu ya baraza hilo imeshirikiana na kamati zake na mamlaka za serikali za mitaa katika kushughulikia changamoto halisi zinazoyakabili mashirika ya kibinafsi.

Kwa kuangalia mbele, Baraza la mashauriano ya kisiasa litaendelea kujikita katika kutoa mapendekezo juu ya sera kuu za Kamati Kuu ya CPC, mahitaji ya mikakati muhimu ya nchi, na masuala makubwa ya maendeleo halisi, ambavyo vyote vinahusiana na malengo na kazi za maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, msemaji huyo amesea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha